NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan amesema hakuna jambo gumu kulitekeleza miongoni mwa ambayo wamekubaliana katika maridhiano na viongozi wa vyama vya upinzani hivyo amevitaka vyama hivyo kutulia na kusubiri matokeo yatakayozalisha Taifa jipya.
Rais Dk.Samia ametoa kauli hiyo leo Machi 08, 2023 kwenye kongamano la siku ya wanawake lilioandaliwa na Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha).
Miongoni mwa msisitizo mkubwa uliotolewa na viongozi wakuu wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Freeeman Mbowe kwa Rais Dk.Samia ni suala la katiba mpya,mabadiliko katika sheria za uchaguzi ambapo zitafanya wananchi kuongozwa na viongozi waliowachagua kwa utashi wao.
Akijibu hoja hizo Rais Dk.Samia amesema hakuna kisichowezekana katika mazungumzo japokuwa si utamaduni rahisi lakini kila jambo utekelezaji wake utakuja taratibu.
“Hakuna kisichowezekana kwenye mazungumzo najua si rahisi kwa utamaduni huu kwangu kuna vikwazo kwenu, nasomaga Jamii Forum mnavyocharurana wengine Wanasema Mbowe kalamba asali hawa ndo wahafidhina wasiotaka marrishiano,nasema huu ni utamaduni mpya si rahisi kukubalika haraka”
“Hata katika chama changu nilipopendekeza kufungua mikutano ya hadhara kulikuwa kugumu kidogo,kwa hiyo wahafidhina wapo kwako na kwangu watatuelewa tu lengo kubwa kujenga amani ya nchi yetu,”amesema Dk.Rais Samia.
Amesema katika ubunifu wake wa kisiasa amechagua njia ya maridhiano hivyo mambo yote yatakuja polepole.
“Mageuzi yapo na tutajenga Taifa jipya,Taifa lenye uchaguzi wa ushindani na si vurugu”
“Yaliyosemwa hapa yote yatafanyika hakuna gumu pale,katiba hakuna anayelikataa,au muda mrefu tutatangaza kamati kwakushirikiana na viongozi waanze kufanya kazi hiyo,kuhusu wabunge 19 mmeshasema lipo Mahakamani tuachie mkondo ule uendelee tutazame yanayokuja si rahisi mimi kutia neno hata kama ni rais,”amesema Rais Dk Samia.
Amesema mazungumzo ya maridhiano ni endelevu hivyo watakwenda mpaka watafika panapohitajika.
Amesema siasa ni mchezo wa fikra na mawazo wote wana lengo la kushika dola
“Kwa sasa najua Hamna mawazo yakushika dola mnajua mama yupo tufanye siasa za kistaarab kwakuwa katika kipindi hiki kifupi nchi yetu inaheshimika sana,”alisema Dk.Samia.
Kuhusu kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo Dk.Samia amesema wananchi wanasema haijapata kutokea lakini kwako yeye ni faraja
“Tumeandika historia mpya katika jitihada yakuliunganisha Taifa,nilipopata mwaliko wa kuwa mgeni rasmi BWacha sikusita na sikusita kwa sababu mimi ni rais kwa hiyo hili kundi ni kundi langu pia .
“Huwezi kuitwa na wananchi wako ukasema siji haiwezekani,lakini nilifurahi kuja pia kwa sababu nilijua leo nitasikia Chadema wanasema nini ,na kwakweli nimesikia wanawake wa Chadema wanasema nini na nimesikia Chadema kama chama kinasema nini,”alisema Dk.Samia.
Akizungumzia kuhusu siku ya wanawake alisema lengo la serikali na wanawake kwa ujumla ni kuhakikisha mwanamke wa Tanzania anathaminiwa na kupewa Haki Kama mwanamke yoyote Duniani.
“Historia yakupambana na mambo ya wanawake ni ndefu changamoto zetu ni nyingi ukiacha huku kunapotupiwa lawama kwenye serikali siasa na mambo mengine mila tamaduni na makuzi yetu na mengine
Changamoto hizi zinawapata wanawake wote wa Tanzania
Changamoto hizi hazichagui itikadi yaki siasa wala dini,Kama tunapigwa ni wote,Kama michepuko wote chakufanya hii nguvu ya watu ikaungane na kila mwanamke tukamkomboe mwanamke wa Tanzania,tukakuze uchumi wa mwanamke wa Tanzania,mkianza kuweka mipaka hatutafika .”amesema.
Kwa upande wa Mbowe amesema anatambua kuwa maridhiano kwa nchi hayawezi kuwa ya vyama viwili tu kwa maana ya Chadema na CCM hivyo vipo vyama vingine vya kisiasa zipo taasisi nyingine za kiroho na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali.
“Wapo wakulima,Wapo wafanyakazi wapo makundi mengi hatimaye sasa tukimaliza kuweka misingi ni lazima mchakato uende mbele kushirikisha maridhiano yote ya Taifa zima na watanzania wote wa imani zote ili kwa pamoja tuweze kujenga Taifa bora lente furaha .
“Nilipotangaza ujio wako kwenye kongamano la Bawacha wengi waliamini pengine ni utani,wengi waliopokea kwa hisia tofauti chanya na hasi yote haya ni udhibitisho wa namna Taifa letu linavyoishi kwa hofu,utengano,kutokupendana na kutokuaminiana
Unafiki na uongo ulaanisha Taifa,Taifa letu lina watu wengi wasiosema na kuuishi ukweli ,”amesema Mbowe.
Amesema hali hiyo ni chimbuko kubwa la poromoko la maadili hivyo alimsihi Rais Samia kumuepuka mtu yeyote anayejiita chawa wake.
“Sisi wengine tumechagua kusema ukweli na kukwepa dhambi ya unafki,tumelipa gharama kubwa kwenye hili kwa misingi na misimamo yetu hiyo,tunaamini ukweli uwazi kutokuwa wanafiki ndiyo njia bora yakukusaidia uweze kuwa kiongozi bora na ndiyo bora yakuisaidia serikali yako ili iweze kutekeleza wajibu wako .
“Na sisi kama chama kikuu Cha upinzani tutaishi maisha hayo bila woga wowote,bila unafki wowote,bila kujikomba,bila uchawa tutanyoosha na tutasema Kama inavyostahili kwa sababu tunaamini hiyo ndiyo njia sahihi yakuwatengenezea watoto na watoto wa watoto wetu Taifa bora kwa siku zijazo na kizazi kijacho.
“Hofu hizi lazima tuzimalize kwa vitendo ukiwa mkuu wa nchi ukawa mkatili mfumo mzima wa utawala wako unakuwa katili ,lakini mkiwa na mkuu wa nchi mpatanishi ,muunganishi mfumo wake mzima wa utawala nao hugeuka hivyo hivyo
Ni matumaini yangu mheshimiwa rais hadhima yako yakuliweka Taifa pamoja itarithiwa na viongozi waliopo chini yako,”amesema Mbowe.
Amesema ujio wa rais Samia umeonyesha njia namna wanapaswa kusameheana na kwa pamoja kujenga Taifa lenye Uhuru,Haki,demokrasia,maendeleo ya watu wote.
“Demokrasia haipaswi kuwa chaguo hakuna Taifa linalopuuza demokrasia likakumbatia mifumo yenye udikteta,uonevu na dhambi likastawi tunapaswa wakati wote kuwa na viongozi wenye hofu ya kweli ya Mungu na sio ya uigizaji .
“Tunataka viongozi Wetu wawe chaguo halali la watu,wapatikane kwenye chaguzi zilizo huru na Haki na za uwazi hapo tutapata ujasiri wa kusema viongozi wetu ni chaguo la Mungu wataliepusha Taifa letu na laana kubwa
Katiba mpya na katiba bora ndicho kitakachorasimisha maridhiano
Rais na vyombo vyako vyote nawasihi sana msipuuze kauli hii,msione ni kauli ya utani,msione ni kauli ambayo inaweza ikapuuzwa,kauli hii naomba muichukue kwa uzito mkubwa ndiyo sauti na kilio cha Taifa,”amesema.
Amesema pamoja na maridhiano kuahidi katiba mpya na mifumo mipya ya uchaguzi naomba suala hili utekelezaji wake uende haraka.
“Kamwe usiruhusu Taifa kwenda kwenye uchaguzi ujao na mifumo na watu wale wale walioiletea aibu Tanzania na laana kwa Mungu wetu,tukubali Kama Taifa kusema kwa pamoja never and never and never again .
“Maisha tuliyoishi kwa miaka Sita labda wenzetu CCM mnaona Kama utani,hamjui wenzenu tuliishi na roho tumezikamata mikononi yawezekana hata ndani mwenu mliumizana lakini sisi ndo tulifanywa kabisa yaani sherehe zakutuumiza zilikuwa sherehe kwa wenzetu ,yawezekna ndani ya chama chako kuna watu hawataki katiba mpya na tume huru ya uchaguzi hawa hawakutakii amani
Sisi tupo tayari kusamehe na kusahau tulipotoka ,”amesema Mbowe.
Awali Katibu Mkuu wa Bawacha Catherine Ruge alisema wamemualika rais Samia ili ajue changamoto za wanawake wa upinzani na uwezo kuzitolea ufumbuzi.
“Wanawake tunaishi maisha duni
Pamoja na mazuri unayoyafanya tunaamini utafungua sikio lako na kusiikia na kufanyia Kazi yale yaliyo katika utashi.
“Wapo wanaojaribu kukukatisha tamaa wengi wao ni wanaume Bawacha tunasema usiogope
Jitihada za kupata Katiba mpya usiogope maana wanataka ushindwe kama wao walivyoshindwa ,”amesema Ruge.