NA MWANDISHI WETU, KILIMANJARO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wahafidhina (Watu kenye misimamo mikali) wapo kote CCM na Chadema na kumtaka Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe aache kuwasikiliza.
Rais Samia amezungumza hayo Leo Jumatano, Machi 08, 2023 wakati akihutubia kwenye Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha).
Rais Samia alisema alipokaa na washauri wake na kuamua kujenga Tanzania Maya yenye maridhiano, wapo Watu ndani ya chama chake cha Mapinduzi (CCM) na serikalini waliopinga azma hiyo.
Haikuwa rahisi sana, nipata wahafidhina ambao hawakutaka huu muelekeo mpya. Lakini kwa kuwa nilikuwa na dhamira ya dhati, sikutaka kuwapa nafasi wahafidhina hao nikiamini watakuja kuelewa baadae.
Naelewa hata Chadema wapo wahafidhina hao ambao wakti tunakaa na Mbowe kupanga namna ya kufanya, walisema Mbowe amelishwa asali. Nikuombe mwenyekiti kwa pamoja tusonge mbele na tutafika tunapotaka kwenda,” alisema Rais Samia
Pia soma;