NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha KMC FC ya jijini Dar es Salaam, Machi 9, 2023 majira ya saa 10:00 inashuka dimba la Uhuru kuwakaribisha Kagera Sugar ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na ikimkosa mchezaji wake Baraka Majogoro.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Habari wa kikosi hicho, Christina Mwagala na kufafanua kwamba wachezaji, Kelvin Kijiri na David Mapigano wanaendelewa vizuri baada ya kupata majeraha na tayari wamerejea kikosini.
“Timu yetu ambayo iko chini ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana iko katika hali nzuri na kesho tunatawakaribisha Kagera Sugar ya mkoani Kagera ambapo pamoja na mambo mengine mipango na mikakati ya maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa.
“Kocha Msaidizi Ahmad Ally amesema kuwa kama benchi la ufundi limefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kila mmoja yupo tayari katika mchezo huo na kusisitiza kuwa utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba Kagera Sugar inushindani kwani hata kwenye msimamo wa ligi wapo kwenye nafasi nzuri.
” Tunakwenda kucheza nyumbani naamini itakuwa mechi ngumu kwa kuwa tunapresha ya kukosa matokeo rafiki kwenye michezo yetu iliyopita, Ila tumejipanga kukabiliana na presha hiyo bila shaka tutautumia vizri uwanja wa nyumbani,” amesema.
Katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu, KMC FC ilipoteza ugenini dhidi ya Azam kwa bao 1-0 ,mchezo ambao ulipigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi na kwamba katika msimamo inashika nafasi ya 13 ikiwa imekusanya alama 23 na kucheza michezo 24.