Manchester United inafuatilia kwa karibuni mwenendo wa mshambuliaji wa AS Roma, Tammy Abraham. Lakini klabu yake ya zamanı ya Chelsea nayo imeonyesha nia ya kumsajili tena mchezaji huyo.
West Ham UTD
Uongozi wa klabu ya West Ham bado ina imani na meneja wa klabu hiyo, David Moyes. Meneja huyo anaonekana kukalia kuti kavu kufuatia mwenendo mbaya wa klabu yake ambayo inachungulia shimo la kushuka daraja ikilindwa na alama moja tu.
NEWCASTLE UTD
Newcastle United ina uhakika kiungo wake raia wa Brazil, Bruno Guimaraes atasaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomuweka muda mrefu zaidi. Klabu hiyo pia inapambana kumsajili kiungo wa kati wa Leicester City na Uingereza, James Maddison na kiungo wa kati wa Manchester United na Scotland, Scott McTominay.