NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
Majeruhi pekee wa ajali ya basi la mwendo kasi aliyesalia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa( MOI)Osam Milanzi ambaye video ilionesha kuwa ni mtembea kwa miguu aliyegongwa na basi la abiria la ‘Mwendokasi’ wiki mbili zilizopita anaendelea vizuri
Akizungumza ma Demokrasia leo Machi 06, 2023 Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick anesema majeruhi huyu anaendelea vizuri kabisa na hali yake inazidi kuimarika.
Mvungi amesema afya ya Osam imeimarika tangu alipotolewa Chumba cha uangalizi maalum(ICU) wiki iliyopita jambo ambalo ameeleza kuwa ni kazi kubwa inayofanywa na madaktari, viongozi na watumishi mbalimbali wa MOI tangu alipofikishwa hospitalini hapo.
Ajali hiyo ya mwendokasi ilitokea Februari 22, 2023 saa 6:10 mchana katika makutano ya barabara ya Morogoro na Jamhuri, Kisutu Dar es Salaam ikihusisha basi lenye namba T122 DGW aina ya Dragon mali ya kampuni ya UDART.
Basi hilo lilikuwa likitokea Kivukoni kwenda Kimara ambalo liligongana na gari ndogo lenye namba za usajili T978 DHZ aina ya Toyota Avanza mali ya Shirika la Ndege la Rwanda.