NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TAASISI ya Mifupa Muhimbili (MOI) imefanikiwa kumfanyia upasuaji wa kichwa kikubwa mtoto mwenye umri wa wiki moja.
Upasuaji huo umefanywa katika kambi maalum, ambapo zaidi ya watoto 24 wamefanyiwa upasuaji wa kuzibua njia za maji kichwani na kuwekewa mirija ya kutoa maji kichwani na kuyapeleka Tumboni.
Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu katika Taasisi hiyo Dk Hamisi Shabani amesema wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa mtoto mwenye umri mdogo kutokana na uwepo wa wataalam wabobezi na vifaa vya kisasa vya teknolojia ya juu katika taasisi hiyo.