NA MWANDISHI WETU, CHALINZE
WATU watatu wakiwemo Askari wawili wa kituo cha Polisi Wilaya ya Chalinze na karani wa Mahakama ya Lugoba wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria, Toyota Creaster kuacha njia, kugonga karavati na kisha kupinduka Kijiji cha Mboga Kata ya Msoga barabara kuu ya Chalinze – Segera mkoani Pwani.
Aidha katika ajali hiyo askari mwingine amejeruhiwa,
Ajali hiyo imetokea leo Machi 5, 2023 saa 11:45 Kijiji cha Mboga Kata ya Msoga barabara kuu ya Chalinze – Segera mkoani Pwani.
Kamanda wa Polisi Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea tukio hilo na kutaja gari hilo lenye namba T.323 BAL aina ya Toyota Crester likiendeshwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ndwanga Danstan (28) wakitokea Chalinze kuelekea Lugoba.