NA MWANDISHI WETU, MWANZA
ZIKIWA zimepita siku kadhaa tangu kuachiwa huru kutoka gerezani Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi amefanya ibada yake yake ya kwanza na kutaja kuwa yuko mbioni kuanza kuwaleta hadharani watu maarufu waliofariki kama Steven Kanumba aliyefariki miaka miaka 10 iliyopita
Mfalme Zumaridi amesema hayo Februari 26, 2023 wakati wa ibada yake ya kwanza baada ya kuhukumiwa kukaa gerezani mwezi mmoja licha ya kukaa mahabusu miezi kumi.
Zumaridi amesema hakuna kinachomshinda Mungu kwani kuna mauti aina mbili ambayo mtu hufa kwa kuchukuliwa na Mungu na mauti ambayo ni kiini macho ambapo mtu hufariki kwa kuwekwa pembeni ya mlango licha ya ndugu kulia kwa uchungu na kuwatokea kimiujiza.
“Kuna watu huzikwa lakini huonekana katika mazingira ya kutatanisha hivyo umefika wakati, saa, na majira kuushangaza uso wa dunia kuwarudisha wakiwa hai”,
“Ukimwona Kanumba katokea kwenye uso wa dunia usishangae maana miujiza imetendeka na hutokea sio msukule tena bali atakuwa kwa hali yake ya kawaida”, amesema Zumaridi.
Zumaridi amesema hata akiwa gerezani kuna watu walisema kama Kanumba yupo basi wanaomba awaoe ,huku waumini wakicheka wakiona kama ni jambo la kushangaza na kuwaasa waumini wake kuamini ukuu wa Mungu.
Katika hali ya kawaida waumini wameweza kubaki na maswali yake kusubiri miujiza endapo kweli muigizaji maarufu hapa nchini Kanumba kufufuliwa na Mfalme Zumaridi kwani bado kuna mkanganyiko mkubwa.