Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia, Walid bin Talal Al Saudi ambaye ndiye tajiri mkubwa kabisa nchini humo, Februari 21, 2023 katika jengo la Kingdom Tower jijini Riyadh.
Katika mazungumzo yao, Bw Al Waleed ameahidi kusaidia fedha kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa pamoja na kutoa misaada mingine kwenye tasnia ya Sanaa kupitia taasisi yake ya Al Waleed Philanthropies..
Katibu Mkuu Yakubu aliambatana na Mheshimiwa Ali Mwadini, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia.