NA MWANDISHI WETU
MIAKA ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la michezo mbali mbali ya kubashiri maarufu kama kubeti au mikeka ambayo imewafanya vijana wengi kujipatia fedha kwa haraka.
Fedha hizi kwa wanaobeti hupatikana kwenye nyumba za starehe yaani Kasino, mitandaoni , kwenye maduka binafsi hadi mitaani kwenye fremu za kawaida mitaani maarufu kama vibanda umiza Michezo hii imepata umaarufu mkubwa kiasi kwamba inatangazwa na vyombo vya habari vyote ikiwemo redio na vituo vyote vya runinga .
Ni aghalabu kupita dakika tano bila kusikia tangazo la moja wa kampuni wa mchezo huo ambapo Miongoni mwa Kampuni iliyopo masikioni mwa watu wengi sasa hivi ni Meridian Bet. Katika kusimamia hili serikali ilitunga sheria ya michezo ya kubahatisha sura ya 41 ya mwaka 2003 na kanuni zake.
Akisoma bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2022/2023 Waziri wa fedha Dk Mwigulu Nchemba alisema serikali imebadilisha au kuboresha sheria hiyo ili kuongeza mapato ya serikali ambapo mfano sasa kupata kibali cha kuendesha kubeti michezo ya mpira imepanda kutoka laki tano (500,000) hadi milioni moja (1,000,000) wakati kuendesha bahati nasibu ya taifa imepanda kutoka Sh.5,000 /- kwa mchezo mmoja hadi Sh.50,000/-.
Hii ni nje ya kodi ya zuio ya asilimia 10 ambayo mshindi hukatwa akishinda mchezo na asilimia 25 ambayo mwenye kampuni hukatwa kwenye mapato yake yote kwa mwezi .
Kwa Tanzania bodi ya michezo ya kubahatisha ilionesha kwenye ripoti yake ya mwaka 2021 kuwa mzunguko wa fedha katika sekta ndogo ya michezo ya kubahatisha ilikuwa na miamala yenye thamani ya Sh.Tril 3.17/- na makusanyo ya serikali yalikuwa Sh.Bil.132 /-
Kutokana na michezo hii ya kubashiri kuonekana kuliingizia mapato taifa Demokrasia ilifanya mahojiano na Kampuni ya MeridianBet Tanzania inayotoa huduma za michezo ya kubashiri mtandaoni ambapo Meneja Masoko na Mawasiliano wake Matina Nkurlu anaeleza historia ya Kampuni yake tangu kuanzishwa kwake Juni, 2020,shughuli mbalimbali , Malengo na mchango wao kiuchumi na Kijamii.
Hapa Nkurlu anasema chapa ya Meridian Bet, imesajiliwa chini ya Kampuni ya Bit Tech Limited, ikipewa namba 135726.
Kwa sasa MeridianBet inatoa huduma zake katika mikoa mingi ya Tanzania, ikiwa imefanikiwa kuwafikia wengi kupitia kampeni mbalimbali ikiwamo kufungua maduka katika maeneo mbalimbali.
Baadhi ya maduka hayo ni lile lililopo Tandika Majaribio, Wilaya ya Temeke, Kariakoo, Manzese, Gongolamboto na maeneo mengineo.
SHUGHULI ZA KIJAMII
“Meridian Bet Tanzania inaamini katika kurudisha kwa jamii, hivyo imeshafanya shughuli mbalimbali za kijamii, lakini pia kuwasaidia wafanyakazi wake katika suala zima la kuboresha maisha yao na familia zao.” Anaeleza Nkurlu
Aidha anafafanua kuwa shughuli ambazo kampuni imezifanya hadi sasa ni kutoa misaada mbalimbali, mfano ukiwa ni msaada kwa wanawake wasiojiweza Kibaha, Chama cha Watu Wenye Ualbino (TAS), Hospital ya Tumbi, kufanya usafi ufukweni maeneo ya Kigamboni, kutoa msaada wa komputa mpakato (laptop) katika kituo cha redio cha Radio One na nyinginezo.
AJIRA
Meridian Bet, imefanikiwa kutoa ajira kwa mamia ya watanzania kupitia maduka yetu yaliyopo maeneo mbalimbali nchini, zaidi ikiwa ni jijini Dar es Salaam na mikoa ambayo maduka ya meridianbet yanatoa huduma zake.
HUDUMA
Meridian Bet imekuwa ikitoa huduma bora kwa wateja wake, kupitia njia ya mtandao ambapo wanapatikana kwa tovuti www.meridianbet.co.tz , kwa mfumo wa USSD au moja kwa moja katika maduka yetu, ikiwamo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.Huduma zinazopatikana Meridianbet ni kasino ya mtandaoni, Aviator, Titan Dice, Roullette na mashine za sloti inayotoa nafasi ya kushinda fedha nyingi.
CHANGAMOTO
Anaeleza kuwa , Miongoni mwa changamoto ambazo kampuni imekuwa ikikabiliana nazo na kuzitatua, ni katika kuhakikisha huduma zetu zinawafikia watu wengi zaidi na kwa wakati, kiasi cha kuhakikisha watu wetu wa huduma kwa wateja kwa njia ya mtandani wanafanya kazi saa 24 kwa siku saba za wiki, na kuhakikisha huduma za kubashiri kwa kupitia maduka yetu zinawafikia wateja wetu kwenye maeneo.
MALENGO
Meridian Bet imedhamiria kuwa kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri hapa nchini Tanzania na kutoa huduma bora kabisa na za uhakika, sambamba na kufungua maduka mengi zaidi ili kuwafikia wateja wetu popote walipo.
“Pia, mkakati wetu mwingine ni kuendelea kusaidia jamii kadri ya uwezo wetu, kupitia misaada mbalimbali tunayotoa pamoja na kuzalisha ajira ya mamia ya watanzania” anahitimisha Nkurlu