DAR ES SALAAM
Mkurugenzi mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Helen Kijo-Bisimba amesema Asasi za Kiraia (Azaki) hazipo huru na zimeminywa katika kutekeleza majukumu yake.
Kijo-bisimba ameyasema hayo kwenye Kongamano la maadhimisho ya miaka 75 ya Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu duniani.
Mkurugenzi huyo mstaafu alidai Azaki nyingi zimekufa ama zimepunguza makali ya utendaji wake wa kazi kwasababu ya uwepo wa sheria zinazozibana ama watendaji wake kupokea vitisho kutoka kwa watu wenye mamlaka.
“Bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha sheria ya Asasi za Kiraia inabadilishwa ili kuwapa uhuru wa utekelezaji majukumu yao ya kuisaidia serikali bila kuingiliwa.,
“Hata ibara za haki za binadamu iliingia kwenye katiba ya Tanzania baada ya kazi kubwa waliyofanya wanaharakati kudai mabadiliko hayo” alisema Kijo-bisimba
Kongamano hilo pamoja na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali, liliongozwa na Bakari Machumu kutoka Mwananchi Communications, Rebeca Gyumi wa Msichana Initiative,