NA MWANDISHI WETU
WANUFAIKA wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wameeleza kunufaika na mfuko huo wa fidia na kuwataka watanzania wenye vigezo kujiunga.
Hayo yamebainishwa jana na Beauty Jackson na Halima Sheikh walipozungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano wa WCF kueleza mafanikio ya miaka minane tangu kuanzishwa kwa mfuko huo
Jackson mama wa watoto watatu ambaye mume wake (jina linahifadhiwa)alifariki akiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kazi mwaka 2021 alisema kupitia mfuko wa WCF ameweza kunufaika yeye na watoto wake .
Alisema kupitia fidia anayoipata ameweza kumudu kulipa ada, chakula na mahitaji mengine ya familia yake fungu ambao hulipata kila mwezi na litadumu hadi pale watoto watakapotimiza miaka 18 na yeye atakapofariki dunia.
Kwa upands wake Shekhe ambaye alikuwa dereva wa mabasi ya kampuni ha SuperFeo alisema yeye pia ni miongoni mwa wanufaika mara baada ya kupata ajali mkoani Lindi na kupata ulemavu baada ya mkono wake kukatika.
Alieleza kuwa kupitia mfuko wa WCF alipata matibabu na kuwekewa mkono wa bandia ambao unamuwezesha kumudu kufanya shughuli zake kama kawaida.
Akizungumzia mafanikio ya Mfuko Mkurugenzi Mkuu wa WCF John Mduma alisema anajivunia mafanikio ya miaka minane tangu kuanzishwa kwa mfuko hadi sasa ambapo mfuko umefikia ukuaji wa Sh.Bilioni.346/-
Akieleza zaidi alisema, hadi Septemba 2023, thamani ya Mfuko imefikia Sh.Bilioni 697.5
Mduma alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kujiunga na WCF kwani manufaa ni makubwa na ni mfuko ambao uchangiaji wake ni mdogo na hauna hasara.