NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
HOSPITALI ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa kutoka Japani wanatarajia kuanzisha huduma ya matibabubu ya upasuaji wa kichwa bila kufungua fuvu.
Hayo yameelezwa leo Oktoba 2, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Alphonce Chandika katika mkutano wake na Waandishi wa Habari jijini hapa.
Dk.Chandika amesema kuwa huduma hiyo ambayo ni kwa nadra kuipata nchini na wakati mwingine kwenye mataifa ya nje kwa sasa itapatikana nchini Tanzania na kwenye hospitali ya Benjamini Mkapa.
Mbali na kupatikana kwa huduma hiyo hapa nchini itasaidia kuharakisha upatikanaji wa matibabu na kuokoa gharama ya kutibiwa nje.
Amesema kuwa kwa kiwango kikubwa cha watanzania wanakutwa na ugonjwa wa ubongo ambao unasababishwa na damu kuganda ndani ya mishipa ya kusukuma damu kwenye ubongo na kusababisha mtu kupata kiarusi.
Aidha amesema wagonjwa ambao upata matibabu kwa kufumliwa fuvi la kichwa utumia muda mrefi kupona na kuchukua muda mrefu kwa kuwekwa kwenye chumba mahututi.
Akizungumzia ushirikiano wa Hospitali ya Benjamini Mkapa na madaktari bingwa kutoka nchini Japan amesema ni utekelezaji wa juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye anasisitiza umuhimu wa kujali afya za watanzania.
Dk.Chandika amesema kwa sasa wanaendelea na mafunzo na kupata uzoefu wa kutumia mashine ambazo ni za kiaasa ambazo zinafanya kazi ya kuzibua mishipa ndani ya ubongo bila kufumua fuvu.