NA MWANDISHI WETU, KOROGWE
MKUU wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo mkoani Tanga ametoa msaada wa vifaa vya kujifungulia kwa wajawazito na kuwataka akina mama hao kuvitunza kwani vifaa hivyo ni muhimu kwa ajili ya maandalizi ya kujifungua.
DC Mwegelo alitoa vifaa hivyo Mei 27, 2023 mara baada ya kimalizika kwa mbio za Mamathon zilizofanyika wilayani hapa
Lengo la mbio hizo za Kilometa Moja zilizoongozwa na DC Mwegelo ni kuhamasisha lishe bora kwa wajawazito na umuhimu wa mazoezi.
Mbio hizo zilianzia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe hadi Viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi Manungu, Mjini Korogwe.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mbio hizo za mama wajawazito “MAMATHON” alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UWT) Mary Chatanda.
Hii ni mara ya kwanza Mkoani Tanga kuwepo na Marathoni kwa ajili ya wajawazito.