NA WALTER MGULUCHUMA, KATAVI
ABIRIA waliokuwa wakisafiri na basi leo asubuhi Mei 15, 2023 kutoka wilayani Mpanda mkoani Katavi kuelekea Mbeya wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwamo kutumbukia kwenye Mto Sitalike ambao ni maarufu kwa kuwa na idadi kubwa ya viboko majira ya saa 12:35 asubuhi.
Ajali hiyo imelihusisha basi la Kampuni ya Msingwa lenye namba za usajili T 441 DHZ
Mmoja wa abiria katika basi hilo (Jina linahifadhiwa )chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kutaka kugeuza eneo lenye mlima kurudi nyuma ili kubadilisha njia baada ya kupata taarifa kuwa kuna gari limeziba njia eneo la Lyamba Lyamfipa.
Amesema wanamshukuru Mungu kwani hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa ingawa dereva alitokomea kusikojulikana