NA DENIS CHAMBI, TANGA
WAKULIMA zaidi ya 2000 wa zao la Mkonge waliopo katika vikundi vya Vyama vya Ushirika Wilaya ya Korogwe mkoani hapa wanakabiliwa na ukosefu wa mashine bora kwaajili ya kuchakata zao hilo mara baada ya kutoka shambani.
Hali hiyo husababisha kupata hasara na kuchakata kiwango cha chini ya kiwango licha ya wananchi wengi kuhamasika kujihusisha na kilimo hicho.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Amcos hizo Shedrak Lugendo wakati walipofanya ziara ya pamoja na mkuu wa wilaya Jokate Mwegelo katika Bandari ya Tanga wakiambatana na wadau mbalimbali wa zao la mkonge kuona namna bora ya kuongeza mahusiano katika kuitumia bandari hiyo .
Amesema kuwa uwezekaji mkubwa uliofanywa na serikali bandarini uendane sambamba na kuwainua wakulima wadogo wa zao hilo ili waweze kuzalisha kiwago kikubwa tofauti na ilivyo sasa.
“Viongozi wa Amcos tumefanya jitihada kufanikisha mchakato wa kupata Corona mpya lakini kuna vitu vidogo vidogo ambavyo vinakwamisha mchakato huu ili kuzipata sasa hivi kwa mwezi tani zinazochakatwa ni 500 mpaka 600 lakini kama mkonge utachakatwa inavyotakiwa Amcos kwa mwezi zinao uwezo wa kuchakata tani 1500 sasa serikali imewekeza katika Bandari ya Tanga tunachotakiwa sasa iwawezeshe wakulima wadogo ili na mkonge uliopo usiharibike na kupata hasara” ameongeza Lugendo
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo amesema lengo lilipo sasa ni kuona wanazidi kuhamsisha wanachi wanalima kwa kiasi kikubwa Mkonge na kwa kuwawezesha kiuchumi huku serikali ikiweka mazingira rafiki kwaajili yao pamoja na wawekezaji wa zao hilo ili waweze kuitumia bandari ya Tanga kwa wingi tofauti na hapo nyuma.
Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha alisema maboresho ya bandari hiyo ambayo kwa sasa yamefikia asilimia 99.6 kadiri siku zinavyokwenda milango ya kibiashara inazidi kufunguka na wafanyabiashara kuonesha nia ya dhati kuitumia bandari hiyo hatua ambayo itazidi kuchangia kuongezeka kwa pato la Taifa.
Mmoja wa wawekezaji wa zao la Mkonge Dennis Ruhinda abaye ni mkurugeniz wa uendeshaji katika kampuni ya Ruhinda Limited na wamiliki wa shamba la Mkonge la Mkumbara alisema wamefurahishwa na uwekezaji uliofanywa na serikali katika bandari ya Tanga wao wakiwa ni wanufaika wakubwa wa bandari hiyo bado wataendelea kuitumia na kuwashawishi wawekezaji wengine.

