NA MWANDISHI WETU, TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameutaka Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuharakisha utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kampasi ya Tanga, Wilayani Mkinga Mkoani Tanga.
Msisitizo huo umetolewa na Mkuu Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba alipotembelewa na Uongozi huo kutoka Chuo hicho cha Mzumbe Ofisini kwake leo Mei 4, 2023
” Ni muhimu ujenzi wa kampasi hiyo ya Mzumbe ianze na mapema Wilayani kwani tayari eneno tayari limeshapatikana amefafanua zaidi.
Mradi huo unaokusudiwa kufanyika katika Wilayani hapo kupitia Mradi wa Elimu ya Juu wa Mageuzi wa Kiuchumi (HEET), unafadhiliwa na Benki ya Dunia.
Amesema kuwa Ofisi yake kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa Chuo hicho katika kuhakikisha malengo ya mradi huo yanafikiwa na kuwanufaisha wananchi wa Tanga.
Naye akielezea maendeleo ya mradi huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha amesema, tayari Chuo kimekamilisha Mpango wa Matumizi bora ya ardhi eneo lililotengwa kwa ujenzi, na kutangaza zabuni ya kumpata mkandarasi atakayehusika kufanya tathmini ya athari za kijamii na mazingira, ili ujenzi kuanza.
Ameahidi kuendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa ujenzi pamoja na kuharakisha michakato ya ndani ili zoezi la ujenzi kuanza.