NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BAADHI ya Wakazi wa Jijini Dar es salaam wameeleza juu ya kufurahishwa kwao na promosheni ya UPIGE MWINGI NA AIRTEL KILA MTU NI MSHINDI iliyozinduliwa Mei 3, 2023 jijini hapa.
Miongoni mwa wateja hao ni Mary Msaki ambaye amesema kuwa alizawadiwa SMS 50( kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ) ndani ya saa moja mara baada ya kununua muda wa maongezi wa sh.3, 000 kupitia Airtel money kwenda mtandao mwingine jambo ambalo lilimshangaza na aliipongeza Airtel kwa Promosheni hiyo.
Naye Said Manzi mkazi wa Ukonga amesema awali hakufahamu juu ya promosheni hiyo lakini leo Mei 4, 2023 aliponunua muda wa maongezi wa sh.1000 alizawadiwa Megabaiti 250 kwaajili ya kutazama Airtel Tv jambo ambalo anakiri kushangazwa na promosheni hiyo ya aina yake.
Promosheni hiyo mpya kupitia huduma iliyozinduliwa Mei 3 mwaka huu wateja watajishindia zawadi kabambe pale wanapofanya miamala kwa kutumia mtandao wa Airtel.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua promosheni hiyo ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema ‘ Upige Mwingi na Airtel ni promosheni ya kipekee ambapo kila mteja wa Airtel kwa sasa atapata zaidi pale anakapotumia huduma za Airtel. Kila mtu atajishindia zawadi ya muda wa maongezi papo kwa hapo pale atakapokuwa amefanya muamala wowote au kununua bando
Amesema , wateja wataweza kujishindia zawadi za hapo kwa papo kama vile muda wa maongezi, Pikipiki, TV, Friji na fedha taslimu kuanzia Sh.Milioni 1 hadi 50 kila siku.
Amebainisha kuwa, Sio hivyo tu, kila siku sababu ya kutabasamu kwa wateja wa Airtel kwani sasa kuangalia salio la akaunti ya Airtel Money ni bure kwa wateja wote.
“Kwenye promosheni hiyo ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu, kila mteja wa Airtel anaponunua bando au kufanya muamala wowote kwa kutumia Airtel Money (Kama vile kutuma fedha, kutoa fedha, kulipa bili au Lipa namba) atapata zawadi ya papo kwa hapo ya muda wa maongezi na vile kuingia kwenye droo ya kila siku, wiki na ya mwezi na kujishindia zawadi. ” amefafanua Singano
Aidha Singano ameeleza kuwa wateja anayefanya miamala mingi zaidi anayo nafasi ya kubwa ya kujishindia zawadi. Mawakala wa Airtel Money wanayo nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi pia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Andrew Rugamba aliongeza ‘”Sisi Airtel, tunajali na tumejitolea kuhudumia na kudhamini wateja wetu. Airtel Tanzania ilikuwa Kampuni ya kwanza kuondoa tozo kwenye miamala ya simu kwa wateja wote na sasa ndio ya kwanza kuondoa gharama za kuangalia salio. Hii inaongeza dhamana kwa wateja kwa kila mteja wa Airtel Money na kuwafanya kuwa washindi.”
Wakati huo huo , Airtel kuanzia Mei 3, 2023 imetoa gharama za kuangalia salio ambapo mteja anaweza kupiga *150*60# au kutumia applikesheni ya Airtel, bila gharama yeyote.
Airtel imekuwa Kampuni ya kwanza nchini Tanzania kutoa gharama za kuangalia salio la Airtel Money kwa wateja wote. Ukiwa na Airtel kila mtu ni mshindi!
Lengo la promosheni hiyo ni kuendelea kuhamasisha wateja na mawakala kutumia huduma za Airtel na wakati huo huo kupata nafasi ya kujishindia na Airtel na kuweza kutimiza ndoto zako.
.