TAVETA KUSINI, KENYA
WATU 11 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya basi katika eneo la Taveta kusini nchini Kenya .
Watu hao walipata ajali hiyo walipokuwa wakitoka kwenye mazishi.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu kwenye breki ambapo basi hili lilipoteza mwelekeo na kupinduka.
Ofisa wa Polisi, Morris Okul alisema kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na ukubwa wa ajali hiyo huku akisema majeruhi wanaendelea na matibabu