NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi yatakayofanyika kitaifa mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta) imesema maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani humo ifikapo Mei Mosi.
Kaulimbiu ya mwaka huu itakuwa inasema, ‘Mishahara bora na ajira za staha ni nguzo kwa maendeleo ya wafanyakazi pamoja na kuendeleza kazi.’
Sikukuu ya wafanyakazi duniani hutumika kama fursa ya kuwasilisha changamoto za mfanyakazi kwa mwajiri ili kupata ufumbuzi juu ya changamoto hizo.
Katika maadhimisho yaliyofanyika mwaka jana kitaifa jijini Dodoma serikali iliahidi kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wake kwa lengo la kuwahamasisha wafanye kazi kwa weledi.
Mbali na changamoto zilizoikumba dunia kama Uviko -19 bado Serikali ilipongezwa kwa kuendelea kuwa sikivu kwa kuyafanyia kazi maslahi ya wafanyakazi