NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Aprili 2023.
Taarifa iliyotolewa leo Aprili 8, 2023 na ZURA kupitia kitengo cha mawasiliano imeeleza kuwa bei ya petroli imeshuka kutoka 2,880 hadi 2,780 kwa lita mwezi Aprili.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa mafuta ya Diseli yameshuka kutoka 2,980 hadi 2,900 kwa lita mwezi Aprili.
Bei ya mafuta ya taa imebaki palepale ambapo kwa mwezi Machi ilikuwa 2,921 na mwezi Aprili imebaki kuwa hivyo.
Aidha, mafuta ya ndege yameshuka kutoka 2,681 hadi 2500 kwa lita mwezi Aprili.
Mamlaka hiyo imesema inaendelea kufuatilia na kudhibiti soko la mafuta na bei zake kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha bei za bidhaa hizo haziongezeki maradufu na kutoleta athari katika shughuli za kijamii na kichumi.
ZURA imewataka wananchi kununua mafuta katika Vituo halali vya mafuta na kudai risiti za kielektronika kila wanaponunua.