DENIS CHAMBI, TANGA
WAFANYABIASHARA wa wa vyakula katika masoko ya Mgandini na Ngamiani yaliyopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Tanga wameelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo miundombinu mibovu iliyopo licha ya ushuru wanaotozwa hali ambayo inachangia kuharibika kwa bidhaa zao kabla ya kuuza.
Wakizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman katika ziara yake ya kutembelea, kujua upatikanaji wa bidhaa na hali ya bei ilivyo hususani kipindi hiki katika masoko hayo walisema kuwa pamoja na bidhaa kupatikana na wastani na bei kuwa ya kawaida bado uchakavu wa miundo mbinu imekuwa ni tatizo sugu kwao licha ya viongozi na serikali kutoa ahadi za mara kwa mara kuwawekea mazingira rafiki.
Katibu wa soko la Mgandini Shabani Mohammedi amesema kuwa licha ya wafanyabiashara waliopo katika soko hilo kuchangia sh.9000 kila mwezi kulingana na maelekezo ya Halmashauri ya Jiji la Tanga lakini bado hawaoni faida yake kutokana na kuendelea kufanya baishara zao katika mazingira magumu hasa kayika nyakati za mvua.
“Tuna kilio cha muda mrefu cha kujengewa soko tunalipa ushuru kama kawaida na hakuna mfanyabiashara aliyekataa n tumekuwa tukiahidiwa muda mrefu kujengewa soko lakini halijengwi , ukiachana na hilo kuna malori yanayoingia hapa ni mengi ambayo yanaweza kusaidia kuwezesha kuchangia mapato kwa kulipia ushuru ” amesema Mohammed.
Mmoja wa wafanyabiashara wanaouza viazi katika soko la Mgandini amesema kuwa bidhaa hiyo ambayo wamekuwa wakiipata nje ya mmoa wa Tanga wamekuwa wakikutana na changamoto ya usafiri wakitozwa ushuru kuwa mkubwa kila mahali wanapopita kabla ya kufika sokoni hapo wakiwa na hayimaye kuambulia tu hasara.
“Wateja kipindi hiki cha Ramadhani sio wengi kivile tunakutana na changamoto njiani wakati tunasafirisha mzigo kutoka shambani hasa sisi wa viazi serikali ijue kwamba sisi hatupati faida tunapata hasara tunatozwa ushuru mkubwa njiani na tukifika hapa sokoni viazi vinaoza”
Akizungumza mara baada ya kujionea hali ya upatikanaji wa bidhaa, bei na miundombinu ilivyo katika masoko yote mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Abdulrahman amesema kuwa wamejipanga kufanya ziara katika masoko yote yaliyopo mkoani humo kwa lengo la kujua changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara na kuona namna nzuri ya kuweza kuzitatua kwa manufaa ya wananchi wote.
” Ziara yetu ya leo tumekuja kuangalia hali ya upatikanaji wa bidhaa pamoja na hali ya bei zake lakini nitarudi sasa maalum baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kufanya ziara mkoa mzima wa Tanga na ikiwemo katika mji wa Tanga wenyewe na katika soko hili la Mgandini ndio hasa pana changamoto kubwa soko hili mmeahidiwa kwa muda mrefu na halijengwi miundombinu yake ya hovyo hivyo lazima miundombinu ikae katika hali nzuri ili mraji wa mwisho aweze kufaidika apate matunda ya nchi yake” ameeleza Mwenyekiti huyo na kuongeza
“Nitafanya ziara mahususi katika mkoa mzima wa Tanga kila halmashauri watueleze wamejipangaje kuondoa kilio cha muda mrefu cha wafanyabiashara kuwaboreshea miundo mbinu katika mazingira yaliyo mazuri maana mwisho wa siku ukimboreshea mfanyabiashara unafanya afya ya mlaji nayo iweze kuimarika lakini sio katika hali iliyopo sasa haitulidhishi tunaamini serikali itafanyia kazi ushauri ambao tunatoa” wq
Hata hivyo licha ya kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo awali ilizoeleka kuwa bei za bidhaa na vyakula vingi kupanda lakini katika masoko hayo bei ipo kawaida kama siku zote huku bidhaa zikitajwa kuadimika kutokana na kipindi cha ukame wa baadhi ya maeneo hii ikichangiwa na ukosefu wa mvua za kutosha.