NAIROBI, KENYA
POLISI nchini Kenya wametawanywa kwenye mji mkuu wa Nairobi ili kuwadhibiti wananchi wanaoandamana.
Vizuizi vimewekwa kwenye barabara ya kuelekea Ikulu na kwenye ofisi nyeti za serikali.
Mamlaka zimesitisha huduma za treni jijini Nairobi zikihofia uharibifu unaoweza kufanywa.
Waandamanaji katika miji ya magharibi ya Kisumu, Homa Bay na Migori tayari wamefunga barabara kwa moto na mawe, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
Kumekuwa na mvutano mkali siku za hivi karibuni baina ya wafuasi wa wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga.
Mnamo Jumatatu, shamba la familia ya rais wa zamani Uhuru Kenyatta lilivamiwa na waporaji na kiwanda cha mitungi ya gesi kinachohusishwa na Raila Odinga pia kikaharibiwa.