NAIROBI, KENYA
WANANCHI nchini Kenya wamevamia shamba la familia ya rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kuharibu mazao wakati nchi hiyo ikiwa kwenye maandamano ya raia wakipinga kupanda kwa gharama za maisha.
Wavamizi hao walikata miti kwa kutumia misumeno ya umeme na kuiba mamia ya mifugo wakiwemo ng’ombe kwenye shamba kubwa lililo nje kidogo ya jiji la Nairobi.
Taarifa zinasema biashara karibu na shamba hilo zimefungwa kwa kuhofia kuvamiwa huku eneo hilo likiwa halina ulinzi wa kutosha wa jeshi la polisi.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, aliitisha maandamano nchi nzima akiwa na agenda ya kutaka serikali idhibiti kupanda kwa gharama za maisha.
PIA SOMA: