NA EDNA BONDO, ARUSHA
NABII Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lililopo jijini Arusha Dk GeorDavie amemshukuru Rais Samia kwa kumkaribisha chakula cha jioni Machi 04, 2023.
Nabii Mkuu ameambatanisha shukrani zake kwa Rais Ssmia kwa kile alichokiita ni kuheshimishwa.
Amesema Rais Samia amemuheshimisha kwa kiwango cha juu ambacho hakukitarajia.
Nabii Mkuu Dk GeorDavie ameyasema hayo katika Ibada ya Jumapili Machi 5, 2023 alipokuwa akiwahubiria mamia ya waumini kanisani kwake Kisongo jijini Arusha.
“Nilipata heshima hiyo ya kukaribishwa katika Ikulu ndogo ya Arusha ambapo walikuwepo Mawaziri wote , Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu wote na viongozi mbalimbali” amesema Dk GeorDavie
Katika hatua nyingine Nabii Mkuu Dk Geor Davie ambaye pia ni Balozi wa Amani ameeleza kufarijika kusikia viongozi wakuu wa nchi wakiongelea habari ya msaada wa sh.Mil 100 alioutoa kwa wafanyabiashara wa Soko la Samunge ambao waliounguliwa na mabanda yao miaka mitano iliyopita.
Amesema amefurahi sana kuwaona Mawaziri wakimfuata na kumpongeza na ametumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi wakuu wa nchi kwa kumuheshimu na kutambua juhudi zake.