NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
DIWANI wa Kata ya Mjini Kati Jijini hapa Abdulrasul Tojo amewahimiza wafanyabiashara wa Soko Kuu kulipa kodi mbalimbali kwa wakati .
Aidha amewataka wenye maduka kuhakikisha wanakuwa na leseni kwenye maduka yao ili kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Sambamba na hilo Diwani Tojo amewaomba wananchi kushirikiana pamoja kukemea na kupinga mapenzi ya jinsia moja kwa kuwa huo sio utamaduni wetu na ni laana pia ni kinyume na matakwa ya Mungu na jambo hilo ni hatari sana halifai kuwepo.
Rai hiyo imetolewa na Diwani Tojo,kwenye mkutano wa hadhara wa maendeleo ya kata uliofanyika katika soko hilo, ikiwemo kusoma taarifa ya mapato na matumizi na kusikiliza kero za wananchi .
Tojo amewahimiza wafanyabiashara kwenye Kata hiyo kuhakikisha wanalipa kodi na ushuru ili kuiwezesha Halmashauri hiyo kutoa huduma ipasavyo kwani katika kipindi cha mwaka jana 2022/23 walitenga kukusanya kiasi cha Sh.bilioni 30 ,lakini waliishia kukusanya Sh.bilioni 17 pekee.
Amesema ulipaji wa kodi na ushuru umekuwa wa kusuasua na hivyo kushindwa kufikia malengo wakati soko hilo ambalo lililojengwa miaka ya 1960 lina wafanyabiashara1900 ,lakini mapato yake ni madogo kwani kwa mwezi wanakusanya sh.milioni 48 hadi 50 na linahitaji matengenezo makubwa ya miundo mbinu yake.
Amebainisha kuwa katika bajeti ya mwaka huu kata hiyo itapokea shilingi bilioni 2.5 kwaajili ya shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu ya maji taka na ,mifumo ya masoko ya Samunge na soko kuu pia ukarabati utahusisha shule tatu,za msingi ambazo ni Uhuru na Meru,pia shule moja ya sekondari Arusha
Amewaomba wafanyabiashara kwenye Kata hiyo kuongeza kasi ya ulipaji wa kodi ,ushuru leseni za maduka ambao unasuasua na kuwaambia kuwa halmashauri imeanzisha Kikosi Kazi kukagua kila duka kama wanazo leseni,wamelipa mapato yote kwa mjibu wa sheria kwa kuwa imebainika kuna ukwepaji
Amefafanua kuwa, ukarabati huo utahusisha,uwekaji wa taa za barabarani,ujenzi wa barabara za kati kati ya Jiji kwa kiwango cha lami kwenye mitaa ukarabati wa mifumo ya maji ya mvua na kuzibua mifereji
Katika hatua nyingine baadhi ya wafanyabiashara wa Soko Kuu wamelalamikia kero mbalimbali ikiwemo ukubwa wa kodi za maduka waliopangisha,kutokuwepo na vyoo,pamoja na mitaro ya maji kutoa harufu mbaya kiasi kwamba wateja wamekuwa wakikerwa na harufu hiyo na kushindwa kununua bidhaa,jambo ambalo Diwani Tojo ameahidi kutatua
.