NA MWANDISHI WETU, MBEYA
MWANAFUNZI wa darasa la sita, katika Shule ya Msingi Lyoto, Kata ya Ilemi jijini Mbeya, Ibrahim Edson (12), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani chumbani kwake, chanzo kikidaiwa ni hasira baada ya kukaripiwa na ndugu zake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutolea ufafanuzi.
Mama wa marehemu Ibrahim Edson , Dafroza Edson ameelezea mazingira ya kifo cha mtoto wake, kwamba alimuaga anaenda kulala chumbani kwake, lakini baadaye dada yake alivyoingia chumbani alimkuta tayari kashajitundika kwenye kamba na mauti yamemfika