NA MWANDISHI WETU
TANZANIA inategemea kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hadi Saudi Arabia ambapo safari ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Jeddah inatarajiwa kuanza Machi 26 , 2023.
Hayo yamebainishwa katika mazungumzo ya Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Abdulrahman Alabdulwahab na kujadili maandalizi ya uzinduzi wa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na Saudi Arabia.
Katika mazungumzo yao viongozi hao pia walijadili mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za Tanzania hususan nyama na matunda.