NA MWANDISHI WETU, KILIMANJARO
MTOTO mchanga wa wiki mbili aliyechomwa kisu na kisha utumbo kutoka nje na mama yake kuuawa akiwa amelala, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).
Februari 22, mwaka huu Mwanamke huyo ajulikanaye kwa jina la Fausta Tesha (26) mkazi wa Mero, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro alichomwa kisu sehemu za mwili wake na kisha kufariki dunia huku mwanaye huyo akijeruhiwa tumboni hali ambayo iliyosababisha utumbo kutika nje.
Februari 25, 2023, Mama mzazi wa binti huyo, Ezra Tesha amesema mjukuu wake amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC.