NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
MKUU wa Idara ya Fedha na Uhasibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Deo Fazah amesema vitabu vya kidato cha tano na sita vinapatikana kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba)jijini Dar ES Salaam kwa bei elekezi
Pia amesema Vitabu vyote vya Kiada vilivyofanyiwa maboresho vipo kwenye maonesho ya Sabasaba na maeneo yote.
Aidha amesema kuwa,Taasisi ipo na maduka yake Kikanda, ikiwemo pale Ofisi TET Bamaga, lakini pia Kariakoo na kwa mawakala wengine wote.
Pia amesema wapo Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu Kusini kote huko vitabu vyote vipo na vinauzwa kwa bei elekezi kwa bei ileile ambayo kitabu kinachouzwa Dar es salaam na Kigoma ama Mbeya kitauzwa kwa bei ileile
Aidha Faza amesema Taasisi hiyo ndiyo moyo halisi wa elimu nchini kwa elimu yetu ya Msingi,Sekondari na Ualimu.
Fazah amesema hayo katika Banda la TET ndani ya Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea barabara ya Kilwa, Temeke Jijini Dar es salaam.
“Tunapopata nafasi kama hii, tunashiriki ili kuwaambia Watanzania kile tunachofanya, tunapenda kuwakaribisha wadau wote wanaoweza kujitokeza Kufanya kazi na TET katika uandaaji wa Vitabu vya Kiada.” amebainisha
Mbali ya yote,amewakaribisha wadau wanaotaka kufanya masuala ya Utafiti katika elimu milango ipo wazi katika mashirikiano na TET katika kuendeleza elimu nchini.
“Wazazi, walezi, Wanafunzi na wadau karibuni sana Vitabu vya kidato cha Tano na Sita pia vipo hapa na wote wanaweza kutembelea hapa Sabasaba lakini pia katika ofisi zetu za makao makuu ya TET “amehitimisha Faza

