NA JANETH JOVIN, DAR ES SALAAM
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa wafungwa, mahabusu na wanafunzi waliohukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita wataruhusiwa kuandikishwa kuwa Wapiga Kura.
Hayo yamebainishwa leo Juni 13,2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC, Ramadhani Kailima wakati wa mkutano wa Tume hiyo na Waandishi wa Habari kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kailima amesema kwa mujibu wa kanuni ya 15(2)(c) ya kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za mwaka 2024 tume imeweka utaratibu wa kuwawezesha wafungwa, wanafunzi waliohukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita na Mahabusu kuandikishwa kuwa wapiga kura.
Amesema kwa Tanzania Bara kuna vituo vya kuandikisha Wapiga Kura 130 vilivyopo kwenye Magereza na kwa Zanzibar kuna vituo 10 vilivyopo kwenye vyuo vya mafunzo.
Aidha amesema ununuzi wa vifaa vya uandikishaji ikiwemo ununuzi wa BVR Kits 6,000 zinazotumia vishkwambi kuchukua taarifa za Wapiga Kura ikiwemo picha, śaini na alama za vidole.
“BVR Kits za sasa zinatumia mfumo endeshi wa android na uzito wake ni 18 kg, awali zilikuwa zinatumia mfumo endeshi wa window na uzito wa Kilogramu 35, hivyo kwa Tanzania bara kuna vituo vya kuandikisha wapiga kura 130 vilivyopo kwenye Magereza na kwa Zanzibar kuna vituo 10 vilivyopo kwenye vyuo vya Mafunzo, “ amesema