NA ATUPAKISYE MWAISAKA,DAR ES SALAAM
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema kuwa Sheria ya kuwaruhusu watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) kupiga kura kuchagua viongozi akiwemo Rais.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Saaam leo Juni 13,2024 na Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC, Ramadhani Kailima wakati wa Mkutano wa Tume hiyo na Waandishi wa Habari kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kailima amesema ikifika wakati sheria ikitungwa basi watawaruhusu diaspora kushiriki mchakato wa uchaguzi na kwamba matumizi ya vitambulisho vingine yatafanyika kadiri mifumo ya kisheria itakavyoona kama kuna urahisi wa kuvitumia.
“Kura zinapigwa na kuhesabiwa katika Majimbo, sasa Diaspora sasa hivi watapiga kura katika majimbo gani, sisi tunasubiri sheria ikitungwa kuhusiana na kundi hilo kushiriki mchakato wa uchaguzi basi tutatekeleza,” amesema