NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
IKIWA ni siku ya 11 (Julai 8, 2026) ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama SabaSaba,viongozi na wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea na kupata elimu ya vipimo katika Banda la Wakala wa Vipimo.
Mbali na elimu, zawadi mbalimbali zenye nembo na jumbe za WMA zinatolewa kwa wadau huku Wakala wa vipimo wakisisitiza kwamba bado watu hawajachelewa hivyo wanatumia fursa hii kuwakaribisha kwa wingi katika banda lao ili kupata huduma zao.




