NA MWANDISHI WETU,DODOMA
MWENYEKITI wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama, ametangaza orodha teule ya waliopendekezwa kuwania tuzo hiyo katika hafla itakayofanyika Aprili 13,2026 katika ukumbi wa Superdom Masaki jijini Dar salaam.
Washindi hao wa kila nyanja wamepatikana kutoka kwenye miswada 260 iliyofanyiwa kazi na Majaji wa tuzo hiyo ikihusisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania pamoja na washiriki wapya kutoka nje ya nchi.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatano Aprili 8, 2026 jijini Dodoma, Prof. Mlama amesisitiza kuwa mwitikio wa mwaka huu umekuwa mkubwa na ni ishara ya hamasa ya waandishi kushiriki katika kukuza fasihi na uandishi bunifu.
Ameongeza kuwa Washindi wa kila nyanja watatangazwa rasmi Aprili 13, 2026 na kuzawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na vyeti.
Ameendelea kusema kuwa, mshindi wa kwanza, muswada wake utachapishwa na Serikali itanunua nakala kwa ajili ya shule na maktaba za taifa ili kuendeleza fasihi na kuhamasisha uandishi bunifu nchini.






