NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 11, 2025 amepokea kwa niaba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan tuzo ya kutambua mchango wake katika kusimamia ustawi wa jamii ya watu wenye ulemavu nchini, kwenye hafla iliyofanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope (FDM).
Akizungumza kwenye tukio hilo Majaliwa amewaeleza kuwa Rais Dk. Samia yupo tayari kuendelea kufanya makubwa kwa jamii hiyo na ataendelea kuwahudumia.