NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
UCHUMI wa taifa hauwezi kuwa wa kizalendo kama haujengi fursa kwa
wananchi wake.

Aidha upendeleo kwa wazawa si dhambi, bali ni mbinu halali
ya kiuchumi inayotumika duniani kote.
Vilevile uwekezaji unaowashirikisha
Watanzania ndio bora zaidi hivyo ni vyema kushirikisha sekta binafsi katika
mchakato wa kutunga sera ili
kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji wa ndani na kukuza ushiriki wa Watanzania kwenye miradi ya kitaifa.

Pia wananchi wameombwa
Kuepuka kuwadhalilisha wafanyabiashara wazawa kupitia mitandao ya kijamii bali wa natakiwa kutoa malalamiko yao kwa njia rasmi iwapo kuna hoja za msingi.
Haya yanaelezwa na Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania Vincent Minja jijini Dar ES salama leo Jumanne Septemba 23,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Pendekezo la kuwepo kwa Sheria na Sera zitakazotoa Kipaumbele ili kulinda maslahi ya wazawa.
“Wafanyabiashara hawa wanatoa ajira, wanachangia mapato ya serikali, na
wanahatarisha mitaji yao kwa ajili ya maendeleo ya taifa. Tuwaunge mkono
badala ya kuwakatisha tamaa,” amesisitiza Minja.

Minja amebainisha kuwa licha ya uwepo wa sheria zenye msingi mzuri bado zinahitajika kuboreshwa kwani ni wakati muafaka sasa kwa taifa kuwa na sera
zenye kuvutia wawekezaji wa ndani .
Minja ametoa mifano ya kimataifa ikiwemo
Wazawa wanapewa zaidi ili kuhakikisha ushiriki wa Watanzania katika miradi mikubwa ya
TCCIA
Amejinasibu kuwa sheria kama vile:
Sheria ya Ununuzi wa Umma (PPRA)
zimeweka msingi wa kulinda wazawa, lakini utekelezaji wake unahita
msukumo mpya ili kuhakikisha Watanzania hawabaki watazamaji katika uchumi
wao.

Ameeleza kuwa ni muhimu sasa kuweka mifumo ya kisheria
na sheria mahsusi zinazolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi.
” Tunakabiliwa na changamoto ya ushiriki mdogo wa Watanzania katika miradi ya usawa wa kiuchumi hivyo basi Uhuru wa
kiuchumi unakuwa wa dhati na wenye tija. ” ameeleza Minja
Ametanabaisha kuwa ,Sekta binafsi ni injini ya uchumi na kwa
kulindwa, itaendelea kusaidia maendeleo jumuishi ya taifa.
Wakati huo huo Minja alitumia fursa hiyo kuipongeza sekta binafsi kwa mchango wake ambapo amesema;
“Haya ni mafanikio yanayoonesha kuwa sekta binafsi ikipewa nafasi inaweza”

Katika hatua nyingine Rais huyo wa Chemba ya Wafanyabiashara hapa nchini ametumia fursa hiyo kutoa
Shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita
TCCIA imempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi, na kuweka mazingira
wezeshi kwa biashara na uwekezaji.
“Tunatambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuweka mazingira
rafiki kwa sekta binafsi, na tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu kwa manufaa”amesisitiza
Naye Mwanachama wa TCCIA Maeda Waziri ameiomba Serikali kuharakisha michakato ya malipo kwa wawekezaji wazawa wanaofanya kazi na Serikali

