π Asema Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa wanapata haki na heshima
wnayostahili
πAzindua Mpango kazi wa Kitaifa wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama
π Unalenga kushirikisha wanawake kikamilifu katika masuala ya Amani na Usalama
π Ataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutokomeza dalili zinazoweza kuleta
uvunjifu wa amani na usalama katika jamii
π Asema kuzinduliwa kwa mpango kazi wa Amani na Usalama kunaonesha
jinsi Tanzania inavyoheshimu na kutekeleza makubaliano ya kimataifa
NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema
Wanawake ni chanzo cha msukumo wa maendeleo katika Jamii hivyo
Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa kila mwanamke nchini awe mama au
mtoto wa kike anapata haki na heshima anayostahili.
Wakati Serikali ikiendelea kuhakikisha kuwa Wanawake nchini wanapata
haki zao ikiwemo ya usalama na amani, ametoa wito kwao kuendelea
kujitambua na kuchangamkia kila aina ya fursa inayojitokeza nchini.
Dk. Biteko amesema hayo wakati akizindua Mpango kazi wa Kitaifa wa
kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025 β 2029 ikiwa ni
Azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu
Wanawake, Amani na Usalama.
Azimio hilo ambalo limeridhiwa na nchi zote Wanachama wa Umoja wa
Mataifa ikiwemo Tanzania linasisitiza na kutoa kipaumbele kwenye
ushiriki kamili wa wanawake katika hatua zote za ujenzi wa amani,
uzuiaji na utatuzi wa migogoro, mazungumzo ya amani, ulinzi wa amani
na ujenzi mpya wa jamii baada ya migogoro.
.
Dk. Biteko amesema kuwa kutekelezwa kwa Azimio hilo la Umoja wa
Mataifa kunaonesha kuwa Tanzania si nchi inayoridhia tu mipango ya
kimataifa inayowekwa bali inaheshimu makubaliano na maazimio ya
kimataifa na hii inaifanya Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Dk.
Samia Suluhu Hassan nikuzidi kuaminika Kimataifa na kuwa mfano wa
kuigwa.
Akizungumzia, utekelezaji wa Ajenda hiyo ya Wanawake nchini Tanzania,
Dk. Biteko amesema kuwa “Tanzania tulishapiga hatua kubwa na
tunaendelea vizuri katika kutekeleza Ajenda hii ya Wanawake, Amani na
Usalama ambapo kwa mujibu wa Gender Inequality Index ya mwaka 2021,
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilishika nafasi ya 146 kati ya nchi
191 kutokana na maendeleo yaliyopo tangu miaka ya 1990 katika kuhimiza
usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, kubiresha afya ya Mama na
Mtoto pamoja na uwepo wa Uwakilishi wa Wanawake Bungeni.”
Ameongeza kuwa, mujibu wa Global Peace Index ya mwaka 2021; Tanzania
ilishika nafasi ya 58 kati ya nchi 163 zilizo na hali bora ya amani
Duniani.
Akieleza kuhusu mafanikio.mengine yaliyofilkiwa katika Ajenda ya
Wanawake, Amani na Usalama nchini, Dkt. Biteko amesema Tanzania
imeendelea kuwapa Wanawake fursa za juu na za Maamuzi ambapo
hadi.kufikia Mei, 2023 Uwakilishi wa Wanawake katika mfumo wa Mahakama
umefikia asilimia 46.6.
Ameongeza kuwa asilimia 22 ya Askari Polisi ni Wanawake na asilimia 30
ya Maofisa Uhamiaji ni Wanawake vile vile, Tanzania Bara ina Mawakili
wa Serikali 785 ambapo kati yao wanawake ni 410 sawa na asilimia 52.
Ameeleza kuwa kwa upande wa Zanzibar, kuna jumla ya Mawakili wa
Serikali 76 ambapo Wanawake ni 34 sawa na asilimia 44 ya Mawakili wote
hivyo kwa hatuo hizo zilizopigwa na Tanzania nchi haina budi
kujipongeza.
Pamoja na mafanikio hayo, Dkt. Biteko amesema kuwa bado kuna masuala
ambayo yanahitaji kupewa msukumo ili kuleta haki na usalama kwa
wanawake kwani takwimu zinaonesha kuwa asilimia 48.3 ya wanawake wote
Tanzania wamewahi kufanyiwa ukatili wa aina mbalimbali, ambapo mwaka
2015 asilimia 65 ya wanawake waliogombea nafasi mbalimbali za uongozi
walikutana na changamoto ikiwemo za matusi huku asilimia 17 ya
wanawake hao wakishambuliwa na asilimia 13 wakiombwa rushwa ya ngono.
Amesisitiza kuwa takwimu hizo zinaonesha kuwa bado kuna kazi kubwa ya
kufanya ili kuinua haki ya mwanamke hivyo mpango huo uliozinduliwa
unalenga kuhakikisha kuwa matendo yasiyo ya haki kwa wanawake
yanatoweka na hadhi ya mwanamke inapanda kuliko sasa.
Aidha, Dk. Biteko amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuutekeleza
mpango huo wa amani na usalama kwa nguvu kubwa ikiwemo kutoa elimu na
kutokomeza dalili zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na usalama
ikiwemo mila na desturi zinazoweza kuleta madhara kwenye jamii,
wahamiaji haramu, unyanyasaji wa kijinsia na matumizi ya dawa za
kulevya.
Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima ametaja baadhi ya vipaumbele vya
Mpango wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama kuwa ni uzuiaji wa
migogoro, ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi kwenye ngazi
zote katika mikataba ya amani na kuwalinda wanawake na wasichana dhidi
ya unyanyasaji wa kijinsia wakati na baada ya migogoro .
Amesema.kuwa mpango huo utaleta matokeo chanya kwenye masuala ya amani
na usalama kwa wanawake na kuwezesha Serikali kutimiza wajibu wake
kitaifa, kikanda na kimataifa katika kuhakikisha wanawake wanashiriki
kikamilifu kwenye masuala hayo ya amani na usalama.
Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, M
Stergomena Tax amesema uzinduzi wa mpango huo ni tukio la historia na
lenye uzito si kwa taifa tu bali kimataifa katika kujenga dunia yenye
haki usawa na amani.
Ameongeza kuwa, ni kielelezo thabiti cha dhamira ya Serikali katika
ushirikishaji wanawake katika masuala ya amani na usalama na uongozi.
Amemshukuru Rais Samia kwa kuwa sauti ya kimataifa katika kuhakikisha
kuwa Dunia inakuwa na haki na amani na hii imepelekea Tanzania
kutambulika duniani kwa kutoa mchango mkubwa katika misheni za kuleta
amani ambapo hadi sasa Tanzania imeshatoa takriban askari 1500 katika
misheni za kuleta amani na idadi hiyo ikijumuisha wanawake na wanaume.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Zanzibar,
Riziki Pembe ameeleza kuwa Mpango wa Ajjenda ya Wanawake, Amani na
Usalama uliozinduliwa ni muhimu kwa maendeleo ya wanawake wote na
Tanzania kwani maendeleo yanazidi kuchipua pale kunapokuwa na amani na
usalama.
Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatekeleza ajenda hiyo kwa
vitendo kwani nafasi za uongozi kwa wananwake zimeongezeka, mfano
ukiwa ni uteuzi wa majaji wanawake wasiopungua sita ambapo hapo nyuma
idadi ilikuwa chini ya hapo, pia Serikali inazingatia bajeti za
masuala ya kijinsia kwa wizara zote .
Naye, Anna Mutavati, Mkurugenzi wa UN- Women katika Kanda ya
Mashariki na Kusini mwa Afrika, ameipongeza Tanzania kwa kuzindua
ajenda hiyo ya Usalama na Amani kwa wanawake na kueleza kuwa
inaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika masuala ya amani na usalama
ikiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu amabye ni Rais, Dk. Samia Suluhu
Hassan.