NA MWANDISHI WETU, IRINGA
MJUMBE wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Tanzania Bara Shamira Mshangama akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Vijana na kuwapa hamasa vijana kuelekea uchaguzi mkuu, amefanya kikao cha ndani na kamati ya utekelezaji ya UVCCM Wilaya ya Iringa.
Akiwa katika kikao hiko amesisitiza vijana kujipanga kuelekea kuzitafuta kura za CCM na kukipatia chama ushindi.
Baada ya kupokea fedha hizo Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa Comrade Aisha Mpuya alipozungumza amesema “Mimi pamoja na Watendaji wenzangu tumekubaliana fedha hizi tutazigawa kwa wilaya zote, ili ziweze kusapoti ujenzi wa nyumba za makatibu kwenye wilaya zetu”.