NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MBUNGE wa Jimbo la Sengerema, Tabasamu Hamis, amepongeza uamuzi wa Rais Dk. Samia Suluhu kumteua Mohammed Mchengerwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Amesema kuwa Mchengerwa ni Waziri kiraka ambaye amekuwa mstari wa mbele kushughulikia changamoto mbalimbali kwa wananchi ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana, hususan katika Jimbo la Sengerema.
Aidha, ameeleza kuwa Mchengerwa amewahi kutembelea jimbo hilo na kutoa msaada mkubwa kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kushughulikia masuala ya TASAF na mambo mengine muhimu ya kijamii.