NA AMANI NSELLO,MOI,DAR ES SALAAM
TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetoa wito kwa wazazi au walezi wa watoto wenye tatizo la kibiongo kuwaleta hospitalini hapo siku ya Jumapili tarehe 16 na Jumatano tarehe 19, Februari, 2025 kwa ajili ya uchunguzi utakaofuatiwa na kambi maalum ya upasuaji wa kurekebisha kibiongo kuanzia tarehe 24 hadi 29, Februari 2025 katika Taasisi hiyo.
img src=”https://demokrasia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0042-300×200.jpg” alt=”” width=”300″ height=”200″ class=”alignnone size-medium wp-image-15349″ />
Wito huo umetolewa leo Jumatano Februari 12, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Lemeri Mchome wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano uliopo MOI.
Dk.Mchome amesema kuwa madaktari bingwa watawafanyia uchunguzi wa awali watoto wenye matatizo ya kibiongo na wakaobainika kuwa na tatizo hilo wataingizwa katika kambi maalum ya upasuaji itafanyika kuanzia tarehe 24 mpaka 29, Februari 2025 katika taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu.
“Kwahiyo tunatoa wito kwa siku ya tarehe 16 na 19 kutakuwa na uchunguzi wa awali, tutaomba wazazi wawalete watoto wao wenye kibiongo ili wachunguzwe na hatimaye wapate matibabu stahiki ya kunyoosha mgongo wakati wa kambi maalum itakayofanyika Februari 24 hadi 29 Februari 2025 ” amesema Dk. Mchome
Aidha, Dk.Mchome amesema kuwa MOI imekuwa ikitoa huduma ya upasuaji wa kibiongo toka mwaka 2018 kwa mafanikio makubwa.
Pamoja na mambo mengine, Dk.Mchome amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia MOI vifaa tiba ambavyo vinawawezesha Madaktari kutoa huduma za kibingwa na kibobezi.
Kwa upande wake, Daktari bingwa mbobezi wa upasuaji wa mifupa kwa watoto wa MOI, Dk.Bryson Mcharo ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwawahisha watoto wenye kibiongo hospitalini kupatiwa matibabu mapema ili kuepuka upasuaji usiokuwa wa lazima pia kuwaepusha wagonjwa hao na ulemavu.