NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo ( MOI) Dk. Lemeri Mchome amewashukuru Wadau wote waliojitokeza kudhamini na kuunga mkono mbio za Taasisi hiyo maarufu kama ‘Moi Marathon’ zilizofanyika mapema leo Jumapili asubuhi Septemba Mosi,2024 jijini hapa.
Aidha Dk.Mchome amesema kuwa kundi hilo la jamii bado lina uhitaji maalum katika matibabu hivyo wasichoke kuwaunga mkono
“Ninawashukuru wadau wote waliojitokeza kudhamini na kufunga mkono Moi Marathon 2024 na ninawasihi waemdlee lutudhamini kwani bado watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi wanahitaji matibabu” amesisitiza
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa huduma za Uzazi, Mama na Mtoto Wizara ya Afya Dk. Ahmad Makuhani amewapongeza wadau wote waliojitokeza kuchangia matibabu hayo na kuwasihi Watanzania kuendelea na moyo huo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Insurance ambao ni miongoni mwa wadhamini wa mbio hizo ,Karimu Meshack amesema udhamini wao ni Sera ya kurudisha kwa jamii hivyo basi Shirika la Bima la Taifa litaendelea na utaratibu huo kwaajili ya kuisaidia jamii.
“Sisi NIC Insurance tumekuwa na utaratibu ambao upo kwenye Sera yetu ya kurejesha kwa Jamii hivyo basi tutaendelea na sera hiyo kwa manufaa ya jamii” amesisitiza Meshack
MOI Marathoni 2024 ilipambwa na shangwe ‘ya kutosha lililotawala katika mbio hizo maarufu nchini ambapo njia zote tatu zilifurika umati mkubwa wa wakimbiaji wa Kilometa tano,Kumi na 21.
Mbio hizo zimejumuisha watu wa rika zote ikiwemo watoto na wazee walioonekana wakifurahia mazoezi mepesi sambamba na viburudisho mbalimbali.
MOI Marathon ni mbio zinazofanyika kwa msimu wa nne mfululizo ambapo lengo kuu ni kuchangia matibabu ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi asasi ya MO Dewji Foundation ambayo imetoa udhamini wa matibabu kwa watoto 100 na hivyo kuifanya mbio hiyo ifanikishe lengo lake kwa asilia 100.