NA DANSON KAIJAGE,DODOMA
IMEELEZWA kuwa mmomonyoko mkubwa wa maadili na masuala makubwa ya unyanyasaji unasababishwa kwa kiasi kikubwa na akina Mama kushindwa kusimamia malezi na kutokuwa karibu na watoto wao kwa kukosa muda wa kutosha wa kukaa na familia.
Hayo yameelezwa na Mhubiri Anitha Katto,alipokuwa akihubiri katika ibada maalumu ya kilele cha wiki mbili za akina mama yaliyofanyika katika kanisa la Calvary Assemblies of God,(CAG) Mtaa wa Chamelo Nzuguni “B”Jijini Dodoma.
Ibada hiyo ambayo pia katika kutimiza kilele iliambatana na kumpatia zawadi mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Silvester Kamala na familia kwa kuwapatia zawadi ya vigae vya kutandika chini (Taillis) vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.6.
Mhubiri huyo amesema ili kuondokana na mmomonyoko wa maadili kwa watoto ni lazima wazazi na walezi ni lazima karibu na watoto wao kwa ajili ya kutambua changamoto wanazokabiliana nazo na makundi wanayoshirikiana nayo.
Sambamba na hilo amesema kuwa akina mama wengi wanakosa maarifa ya Kimungu ya kumjua Mungu vizuri kwa kujifunza Neno la Mungu kwa kusimami maadili mema ndani ya familia na kusababisha kuwepo kwa mfarakano na kusababisha watoto kuingia mitaani.
Wakati huo huo umoja wa wanawake wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Mlima wa Nuru lililopo Chamelo mtaa wa Nzuguni “B” jijini Dodoma wameitimisha kilele cha wiki mbili za wanawake wa kanisa hilo kwa kufanya maombi maalumu kwa kuombea uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Umoja huo ukifanya ibada ya maombi maalumu ya kuliombea taifa,Uchaguzi wa Serikali za mitaa,Uchaguzi Mkuu wa kuwachagua Madiwani,wqbunge na Rais pia wameomba uchaguzi huo uwe uhuru na haki na pasiwepo vurugu za aina yoyote nchini kama yalivyo Mataifa mengine.
Wakiendelea na maombi wanawake wa kanisa hilo wamesema akina mama wakiwa ni jeshi kubwa ni vyema wakashikamana kwa ajili ya kupaza sauti kwa nguvu kwa ajili ya kumwomba Mungu aweke utulivu na ulinzi kwa ajili ya kuliombea kanisa,kuliombea taifa pamoja na kuendelea kuwaombea viongozi mbalimbali.
“Akina mama ni nguvu kubwa kwahiyo ni wajibu wetu kuunganisha nguvu kuliombea taifa,Viongozi pamoja na kulinda amani ya nchi kwani bila mwanamke kusimama katika zamu yake anaweza kusababisha mmomonyoko wa maadili.
“Kauli mbiu ya wiki ya wanawake inasema ‘Mwanamke mwenye maadili mema’ kutokana na kauli mbiu hiyo ni wajibu wa kila mwanamke anasimama katika maadili na kufanya kazi kwa kusimamia makusudi ya Mungu”amesema Anitha Katto.
Ibada hiyo ya wiki mbili ya kilele cha akina Mama iliambatana na kumtia moyo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Silvester Kamala na familia yake.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa akina mama Juster Mutasingwa amesema kuwa kati ya zawadi zilizotolewa ni pamoja na vigae vya kubandikachini (Tiles) zenye thamani ya Sh.Milioni 1.6.
Juster amesema wiki ya akina mama ambayo ufanyika mara moja kwa mwaka uambatana na zawadi mbalimbali za kumtegemeza Mchungaji kiongozi wa Kanisa la pamoja kulingana na utaratibu wanaokuwa wamejipangia