NA DANSON KAIJAGE,DODOMA
KIKOSI cha Usalama barabarani kimesema mmiliki wa chombo chochote cha usafiri wa moto ambaye hatakisajili kwa hiari ifikapo Septemba 30 chombo hicho hakitaruhusiwa kutembea barabarani na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki.
Hayo yamebainishwa na leo 21 Agust 2024 na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania DCP Ramadhani Ng’azi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma juu ya maandalizi ya wiki ya usalama barabarani ambayo yanatarajiwa kuzinduliwa tarehe 26 Agasti mwaka huu.
Uzinduzi wa wiki ya Usalama barabarani utaambatana na shrehe ya kuadhimisha miaka 50 ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na inatarajiwa mgeni rasm atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango na yatafanyika kitaifa Jijini Dodoma.
DCP Ng’azi amesema wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu itakuwa ya kitofauti zaidi kwani itajikita katika kutoa elimu kwa waendesha vyombo vya usafiri vya moto na kufanya ukaguzi kwa kutoa stika ambayo itakuwa imetambulisha uhakiki wa ukaguzi katika chombo husika.
Amesema wamiliki wote wanatakiwa kutumia wiki hiyo kusanya ukaguzi wa vyombo vyao kwani kama mmiliki hata fanya ukaguzi na kupata stika chombo chake hakitaruhusiwa kutembea barabarani na hakikamatwa hatua kari za kisheria zitachukuliwa.
Akizungumzia kuhusu elimu katika wiki hiyo amesema kwamba watakutana na makundi mbalimbali ya waendeshaji wa vyombo vya moto na kutoa mafunzo juu ya matumizi bora ya usheria za barabarani na umuhimu wa kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto.
“Kwa sasa tumeshuudia ongezeko kubwa la pikipiki za magurudumu mawili maarufu bodaboda lakini waendeshaji wwngi wamekuwa hawafuati sheria sheria za barabarani na wakati mwingine kusababisha ajali
“Kwa kubaini hilo tutakaa na waendesha bodaboda pamoja na waendesha bajaji ili kuwapatia elimu ili watambue umuhimu kuepusha ajari ambazo zimekuwa zikisababisha kupunguza nguvu kazi ya taifa”amesema DCP Ng’azi.
Pia kiongozi huyo ametoa rai kwa waendesha bodaboda kuhakikisha pikipiki zote zikiwa na vifaa vyake vyote vinavyotakiwa kwani ikibainika pikipiki imeondolewa baadhi ya vifaa haitaruhusiwa kutembea barabarani.
Amesema Kikosi cha Usalama barabarani kinatamani kuona kuanzia mwezi Januari hadi Desemba hakuna ajali yeyote ambayo inajitokeza kama kila dereva atafuata sheria ya barabarani.
Wiki ya usalama barabarani ambayo imeandaliwa kitofauti kabisa na miaka mingine ina kauli mbiu yake isemayo “Endesha salama fika Salama”.