NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
WAKALA wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wakulima nchini pamoja na wazalishaji wa bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo kusajili nembo ‘Brand’ za bidhaa zao ili kuzilinda zisichakachuliwe.
Ofisa Usajili kutoka wakala huo Gabriel Barangay, ametoa wito huo , wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu shughuli mbalimbali zinazaofanywa na BRELA, kwenye maonesho ya 31 ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Aidha, Barangay amesema Wakulima wengi nchini wanalima mazao na kuongeza thamani lakini hawana usajili wa nembo za bidhaa zao zitokanazo na mazao ya kilimo.
“Wakulima ni wadau wetu muhimu sana kwani wngi wa wanalima mazao kama mahindi na kuongeza thamani kwa kusaga unga na kufungasha kwenye mifuko lakini wengi wao hawana usajili wa majina ya nembo za bidhaa zao hivyo tunatoa wito kwao kuja kwetu ili kupata usajili ya ‘brand’za bidhaa zao”amesema.