NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la Kituo cha Stesheni ya Reli ya Kisasa ya Dodoma kuitwa jina lake ikiwa ni muda mfupi baada ya kugomea ombi hilo kwa maelezo kuwa bado atafikiria ni Kiongozi gani atapewa jina la stesheni hiyo.
Rais Samia amechomoa ombi hilo lililotolewa na Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania(TRC) kumuomba kituo hicho cha Dodoma kiitwe Jina lake kama heshima ya kuzindua Reli hiyo.
Hata hivyo muda mfupi baada ya kumaliza hotuba yake amesema kuwa amepata majina ya baadhi ya stesheni kulingana na wataalamu walivyo muelekeza.
Vituo hivyo vimepata majina kwa mtiririko kwa kueleza kuwa kituo cha Dar es Salaam kitaitwa jina la Magufuli,Kituo cha Morogoro kitaitwa Kikwete,Kituo cha Dodoma kitaitwa Samia wakati kituo cha Tabora kitaitwa Mwinyi ,kituo cha Shinyanga kitaitwa Abeid Karume,Mwanza Nyerere na Kigoma kitaitwa Mkapa.