NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema uhusiano uliopo kati ya Msumbiji na Tanzania ni wa ukaribu na urafiki.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Julai 4, 2024, alipokutana na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi aliyefika Ikulu Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza ziara yake ya kitaifa ya siku nne nchini.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Rais Nyusi kwa kuitembelea Zanzibar.
Kwa upande mwingine Rais Nyusi ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi , pia amekuja kuaga kabla ya kumaliza muda wake wa Urais.
Msumbiji inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu wa Rais Oktoba mwaka huu pia ametoa mwaliko kwa Rais Dk.Mwinyi kuitembelea Msumbiji kabla hajamaliza muda wake madarakani.