NA JANETH JOVIN, DAR ES SALAAM
RAIS wa Guinea Bissau, Umaro Embalo’ amesema kuwa wanafunzi katika nchi yake wapo tayari kujifunza lugha ya kiswahili na kwamba yeye atakuwa mwanafunzi wa kwanza kujifunza lugha hiyo adhimu ya kiafrika.
Rais Embalo’ ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yake na Rais wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.
Amesema nchi yake itawaleta wanafunzi kutoka Guinea Bissau kuja Tanzania ili wajifunze lugha hiyo adhimu ya kiafrika.
“Lugha ya kiswahili ni nzuri, nitawaleta wanafunzi wa Guinea Bissau kuja kujifunza hapa Tanzania na mimi nitakuwa mwanafunzi wa kwanza kujifunza Kiswahili hata hivyo tayari ninafahamu maneno machache ya kiswahili,” amesema Rais Embalo’