Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amesema nahodha wa timu hiyo, Kylian Mbappe amepata jwraha puani katika ushindi wao mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Austria jana Jumatatu.

Kwenye mchezo huo ambao Ufaransa ilipata ushindi huo mwembamba wa bao la kujifunga wapinzani wao mchezo yliopigwa mjini Düsseldorf, Mbappe alipiga mpira kwa kichwa na uso wake ukagonga bega la Kevin Danso na kupelekea kupata jeraha hilo.
Keraha hilo lilimfanya atolewe na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mkongwe, Oliver Giroud.

Kwingineko Slovakia ilishangaza dunia katika mechi yao ya ufunguzi ya Euro 2024 baada ya kuibwaga Wabelgiji katika Kundi E kwa kuwashinda bao 1-0 katika mchezo uliopihwa jijini Frankfurt.
Kwenye mchezo huo, magoli mawili ya Romelu Lukaku yalikataliwa na teknolojia ya VAR.