*Menejimenti ya Wizara yamtaka Mkandarasi wa mradi kuongeza kasi
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
UJENZI wa Jengo la ofisi ya Wizara ya Madini katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma umefikia asilimia 82 na unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu.
Hilo limebainishwa leo Juni 4, 2034 na Meneja wa mradi huo, Mhandisi Peter Mwaisabula kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambaye ni Mkandarasi wakati akielezea maendeleo ya mradi mbele ya Menejimenti ya Wizara ya Madini iliyomtembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya Madini, Festus Mbwilo amemtaka Mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa mradi huo kwa wakati.
Aidha, Mbwilo amemtaka Mkandarasi kutosita kuwasiliana na Wizara pale wanapokumbana na changamoto yeyote ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo.