NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 21, 2024 ni mgeni rasmi katika kongamano la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA).
Katika Kongamano hilo, watajadili kuhusu miaka mitatu ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Madarakani pamoja na Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Viongozi wengine wanaoshiriki katika kongamano hilo ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi.